Simba 3-2 Mbeya City | Highlights | NBC Premier League 18/01/2023

0Simba SC imepata ushindi wa jasho na damu ikiwachapa Mbeya City mabao 3-2 kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Ilikuwa ni mechi ngumu pande zote, wakianza Simba kwa goli la Saidi Ntibazonkiza dakika 11 lakini Mbeya City wakachomoa dakikaya 13.

Saido akafunga goli la pili kwa Simba, kwa mkwaju wa penati dakika ya 49 na Pape Sakho akafumua bomu la Sugunyo na kuipa Simba goli la tatu dakika ya 56 kabla ya Juma Shemvuni kufunga la pili kwa Mbeya Dakika ya 78.

Katika mchezo huu pia Mbeya City walipata pigo kwa beki wao Samson Madeleke kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 66.

source

Leave A Reply

Your email address will not be published.